Images

AFYA BRAND: KWA UJI BORA KWA AFYA YA MTOTO


                                                    Uji ni wa kawaida kabisa kwa watanzania wengi,Mara nyingi hutumika kama kifungua kinywa au mlo  mdogo wa saa kumi jioni.Uji kwa upande mwingine ni chakula kikubwa kwa watoto wachanga,mara nyingi uji huwa chakula cha kwanza mtoto kujifunza kunywa  baada  ya maziwa,pia hutumiwa sana na wajawazito na wagonjwa.Uji pia ni chakula kikubwa sana kwa baadhi ya makabila,wajaluo wenzangu naamini mtaniunga mkono nikisema bila uji maisha hayasongi.

Unga ndio kiungo kikuu cha uji ,haijalishi unga huo umetokana na nini,unaweza kua  wa mchele,mahindi,maharage,njegere,dagaa,karanga na kadhalika.Ingawa unga wowote huweza tengeneza uji imezoeleka kwa wengi kwamba uji hupikwa kwa unga wa nafaka ambao wanga ndio kirutubisho kikuu ndani yake.

Kwakua unga wa vitu mbalimbali hubeba virutubisho aina tofauti tofauti,ni sawa kabisa kuchanganya unga aina tofauti tofauti ili kutengeneza unga mmoja ulioshehena virutubisho.

Miaka hii ya karibuni unga wa lishe umekua na jina kubwa sana,wajasiriamali wengi na viwanda vingi husindika na kufungasha unga wa lishe.Unga huu hutengenezwa kwa kuchanganya unga wa nafaka na unga wa vyakula  vingine  ili kuupa virutubisho vinavyohitajika katika lishe bora.Unga huu huuitwa lishe kwani kwa mtoto mdogo uji upikwao kwa unga huo ndio chakula chake kikuu,kwa maana nyingine huesabika kama chakula na si kinywaji.

Ingawa unga wa lishe umejaa madukani,ni vyema ukatengeneza unga wa lishe wewe mwenyewe ili kuhakikish mtoto anapatakilichobora.Wafungashaji wengi wa unga wa lishe wamekua ki biashara zaidi,kwani Ingridients(mahitaji yaliyotumika kuandaa unga huo) walizoandika juu ya mifuko si mahitaji kamili yaliyotumika kuandaa unga huo Na matokeo yake ni kufanya mteja anunue kisicho bora.Wengi wataandika karanga,soya na dagaa kama ingridients lakini hawaweki hata tone ,na wakati mwingine wanaweka katika uwiano usiokua sahihi.

Unga wa lishe wa AFYA BRAND ni unga safi kwa watoto ,nasema hivi kwani  nimeona unga huo ukiboresha afya za watoto wa dada na kaka zangu.Uji wa unga huo ni mtamu mdomoni,hata mtoto anakosa sababu ya kukataa uji.Unga huo hupatikana katika ujazo wa kilo moja, kwenye maduka na supermarkets mbalimbali jijini Dar es salaama .Kama kawaida yangu,sisifii chakula adi nikitie mdomoni na kuthibitisha  ubora wake.

Mtoto hujua chakula kizuri na kibaya,na wanapokua wadogo hawajaanza kuongea wao hufanya mambo kwa vitendo.Mtoto anapokataa uji kila siku,badala ya kumkaba (kama muitavyo kina mama)jaribu kumbadilishia unga au uandaaji wa uji wake.Wakati mwingine mtoto anapokataa uji au chakula ni namna yake ya kukwambia chakula ni kibaya au hakipendi,hata ivyo kuna sababu nyingine nyingine zinazoweza fanya mtoto akatae chakula.

Watu wengi huwapa watoto uji na chakula bila kujali uzuri /ladha ya uji huo mdomoni kwa mtoto.Ukiandaa chakula chenye virutubisho vya kutosha alafu kikawa na ladha mbaya,basi juhudi zako hazina maana kwani mtoto hatakula chakula hicho.Ni vyema ukaonja chakula cha mtoto kabla hujampa endapo wewe hutapenda ladha yake basi ujue hata mtoto anauwezekano mkubwa wa kutoipenda.

Unapoandaa uji wa mtoto zingatia uzito wake kutokana na  umri wa mtoto.mtoto wa miezi 7 na mtoto wa mwaka moja uji wao hutofautiana uzito,hii ni kutokana na uhitaji wa mwili wa mtoto.Kiasi cha uji unachompa mtoto pia hutofautiana kutokana na umri pamoja na uzito wa mtoto.

0 comments: